Tuesday, May 22, 2018

ZINGATIA HII KUHUSU INJILI YA SIKU ZA MWISHO:

"Suala si kusema UNAMWAMINI MUNGU... Hiyo haitoshi... Hata Mashetani yanamwamini na yanatetemeka... Swala Ni Je, UNAMUISHIA MUNGU?? Je, UNAISHI MAISHA MATAKATIFU?? Haya Mafundisho Ya NEEMA ILIYOPITILIZA... Yanayolealea Dhambi Na Kuikumbatia Kwa Mgongo Wa Neema NI YA KISHETANI NA HAYATOKI MBINGUNI... Ni Mafundisho Potofu... NEEMA ALIYOILETA YESU, INATUFUNDISHA KUUKATAA UBAYA WA KILA NAMNA, TUPATE KUISHI KWA UTAUWA, HAKI NA KIASI KATIKA DUNIA HII YA SASA ILIYOHARIBIKA.... Fundisho Lolote Juu Ya Neema Lisilokufundisha ULAZIMA WA UTAUWA, HAKI NA KIASI Bali Linalinda UDHAIFU WAKO Ni FUNDISHO LA KISHETANI Bila Kujali Ni MHUBIRI GANI MAARUFU, ANYEHESHIMIKA NA KUKUBALIWA KIASI GANI.... Lazima Tukazane Na Viwango Halisi Vya Neema; KUKATAA UOVU WA KILA NAMNA... KUISHI KWA HAKI... KUISHI KWA UTAUWA... KUISHI KWA KIASI... TENA KATIKA DUNIA HII HII YA SASA... Fundisho Lolote LISILO PROMOTE UTAKATIFU NI BATILI"
I Don't Care Unafurahi Au Umekasirika, Hakuna Utakatifu Wa 50% AU 99.9% Mbinguni... TAFUTA KWA BIDII HUO UTAKATIFU... NO SHORTCUT TO HEAVEN.
Usifikiri Yesu Alitania, "NJIA IMESONGWA, WAIONAO NA KUIPITIA NI WACHACHE"
Yesu Alisema, "JITAHIDI [KAZANA, PAMBANA KWA MAOMBI, NENO NA ROHO MTAKATIFU] KUPITIA KATIKA MLANGO MWEMBAMBA, KWA MAANA WENGI WATATAKA [HAKUNA ASIYETAKA KUINGIA MBINGUNI] KUINGIA LAKINI WASIWEZE"
Hii Ndiyo Injili... Hakuna Kutia Maji... Kuokoka Ni Rahisi Ila kuingia Mbinguni Ni Gharama Kubwa Sana.
Yesu Anasema, "IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA DHIKI NYINGI"
Acha Kusikiliza Propaganda za Watu; Alichosema Yesu [Mwenye Mbingu] Ndicho Sahihi... Hawa Wahubiri Na Wachungaji Na Wote Wengine Ni Watu tu Hawana Mbingu Ya Kukupeleka Hata Wakikupetipeti Kwa INJILI MFU.
I Am Not Ashamed Of The Gospel.