Saturday, September 1, 2018

“MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU MSAADA UTAKAO ONEKANA TELE WAKATI WA MATESO”



“MUNGU KWETU SISI
NI KIMBILIO NA NGUVU
MSAADA  UTAKAO ONEKANA TELE
WAKATI WA MATESO”







BARAKA. A. KAMINYOGE


“MUNGU KWETU SISIS
NI KIMBILIO NA NGUVU
MSAADA UTAKAO ONEKANA TELE
WAKATI WA MATESO”
TOLEO LA1:                                MARCH 2018


                                
Haki zote zimehifadhiwa
BARAKA .A.KAMINYOGE
0758431829,0683903106
DODOMA-TANZANIA
facebook:Baraka andendekisye
email:bandendekisye@gmail.com
youtube:bak man

YALIYOMO
















KIMBILIO LA WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI.
Kimbilio ni mahali palipo na msaada baada ya kupita katika eneo ambalo ni gumu na kushindwa kujiokoa au kujilinda kwa namna yoyote na hapo unapata mahali pa kukimbilia na kusaidiwa iwe ni kiroho au kimwili.
  Kwa mfano mvua ikiwa inanyesha watu hukumbili mahali penye nyumba ambapo wana amini hawawezi kulowana na kuathirika na mvua hiyo katika afya zao. Hivyo hujiokoa afya zao pamoja na mali walizo taka zisilowane na maji ya mvua, kilicho wasaidia ni kimbilio nyumba.
Mfano mwingine wa kimbilio ni huu , Jua linapo kuwa kali mtu yupo njiani kweupe kama jangwani, huwa anateseka na jua sana na mahali pa kukimbilia hakuna inapotokea ameona mti wenye kinvuli mara moja huenda kupumnzika kwa muda ili aendelee na safari tena, wengine japo wana hraka wakifika kwenye mti namna hiyo hutamani wasiondoke hufanya mti kuwa ni kimbilio. Nina amini umeelewa maana ya kimbilio ni mahali pa kujificha usipatwe na baya na ni mahali pa kupata msaada wako.
Watakatifu – ni wanadamu waliopo duniani walio amua kuacha dhambi kabisa na kuwa balozi wa mungu duniani yani muwakilishi wa mungu duniani.
  Watakatifu wa mungu huishi maisha ya toba ,huishi maisha ya wokovu,huishi maisha ya imani,hiushi maisha ya upendo, huishi maisha neno la kristo,huishi kwa kanuni za mungu,huishi kwa kuongozwa na Roho wa mungu,huishi maisha ya kutaka kufikia kimo cha kristo na kutenda kama kristo ila kwa nguvu ya kristo yesu mwenyewe.
Duniani- ni mahali watu walio na mwili wa damu na nyama na viumbe vingine hai vinapatikana (ulimwengu). Katika dunia yapo mambo mengi mema na mabaya ambayo mwanadamu huyaona na kuyafanya ila mtakatifu wa mungu hafanyi yaliyo nje ya mungu. Atendaye kinyume cha mungu ni Yule asiye mtakatifu/ambaye hajamjua kristo.
  Duniani hakuna kuishi milele ni mahali pa kupita tukitoka duniani kuna eneo tutaelekea tena kuishi milele ambako ni mbinguni na jehanamu watenda mabaya wataenda jehanamu watakatifu wa Mungu watakwenda mbinguni.
Ni imani yangu kuwa kichwa cha somo umekielewa vema na ni kwa msaada wa Roho mtakatifu kabisa, kinachosema KIMBILIO LA WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI.
Zaburi 46: 1  Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2  Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
Mambo yanayopatikana hapa
      i.            Mungu kwetu sisi
   ii.            Ni kimbilio
iii.            Ni nguvu
iv.            Msaada unao onekanatele.
   v.            Wakati wa mateso
vi.            Hatutaogopa ijapo badilika nchi
vii.            Hatutaogopa ijapo tetemeka milima moyoni mwa bahari.
i)MUNGU KWETU SISI
Hapa biblia inapo mzungumzia mungu aliye muumba mbingu na nci inaonyesha kuwa ipo miungu mingine  ndio maana ameonyesha umiliki wa “mungu  kwetu sisi” wana mtambulisha mungu wao kuwa huyo mungu ni mungu wa namna gani na ana uwezo gani na kuwa huyo mungu ni tofauti kabisa ni miungu mingine ambayo mungu amewakataza waatakatifu wasi iabudu, kutoka20:4  Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5  Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6  nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kwahiyo biblia inaonyesha kuwa mtakatifu wa mungu aliye hai ndiye watakatifu wanamwamini huyo na hawana mungu mwingine ila yeye ndio maana mungu amewakataza kumwabudu mwingine yeyote. Mimi na wewe kwakuwa tumempokea kristo ndani mwetu ni watakatifu na mungu aliye umba mbingu na nchi ndiye mungu kwetu sisi.
  Huyu mungu kwetu sisis watakatifu tukimwita anaitika, tukimwomba anatupa tuombacho, tukibisha mlangoni anafungua, hujibu sawasawa nakuomba kwetu kwa mapenzi yake, hutu ponya magonjwa,hutusaidia kwenye shida,hutusamehe maovu, hutuinua toka chini kwenda juu, nafsi iliyo inama huiinua tena.
Amua ndani ya moyo wako kumwamini huyu Mungu mwokozi awe wako na ukiwa na shida yoyote ipeleke kwake naye atafanya. Mwandishi zaburi alipoona amemtumia mungu na mungu akamjibu akasema  Zaburi 46: 1  Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2  Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
Maana alimwona wazi wazi , namimi nina amuru imani ipandwe ndani mwako ya kumwamini huyu bwana mwenye nguvu hodari wa vita akupigania katika kila hatua ufanyayo kwa jina layesu ,yoshua24: 14  Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana.
15  Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
 amen.
iI) MUNGU KWETU NI KIMBILIO
Ukiokoka  mungu anakuwa kimbilio kwako maana huna mkuu mwingine zaidi yake yeye mungu aliye umba mbingu na nchi.
Mtoto ana amini kuwa yeyote akimpiga akimwambia baba au mama au mlezi yeyote hufanyika kuwa msaada ndio maana anakimbilia kwake , hivyo tunaye baba wa kiroho ambaye ni mungu tukimwambia haja zetu yeye husikia na kufanyika kuwa msaada kwetu. Usiangaike kuwa ni miungu mingine unapoteza muda maana yupo mungu mkuu mungu wa kweli asiye shindwa na lolote amesema tuombe kwake lolote atatenda yote yohana15: 6  Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
7  Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Iambie nafsi yako na moyo wako umpokee mungu ndani yako ili awe kimbilio kwako na akupe kile utakacho sawasawa na kuamini kwako, hii nafasi ya mungu kuwa kimbilio kwako sio ya kawaida maana wako wanao kwenda kwa waganga lakini nako hapajawa kimbilio la matatizo yao kabisa , wamekimbilia mizimu wamebaki wakiangaika na kuteseka lakini walipo amua kukimbilia jina la yesu wakawa salama.
Omba maombi haya mwambie bwana yesu fanyika kuwa kimbilio kwangu na uwe karibu nami niombapo lolote unipe kwa mapenzi yako katika jina la yesu aimeni.  Yohana14:12  Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
13  Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
ii)Mungu kwetu ni nguvu
Mfanye  mungu kuwa ni nguvu kwako ili uweze kuishi maisha ya utakatifu jinyenyekeze chini ya mungu ili msaada wa mungu usikupite kwa njia ya utakatifu. Ukimtegemea mungu kuwa nguvu kwako unao uwezo wa kushinda kila jaribu kil jambo ambalo wengine wanashindwa kufanya walio mtegemea mwanadamu maana imeandikwa yeremia17: 5  Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6  Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7  Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
iv)Msaada unao onekanatele
Mungu ni msaada kwako ukimtegemea na kumwamini, amua ndani ya moyo wako mungu awe msaada kwako tangu leo ili uishi maisha ya kumpendeza yeye na uwe salama maada kila utakalo kwa msaada wake litafanyika usitumie akili yako muda mrefu mwambie bwana nae atafanya kwa haraka mno maana msaada huwa huchelewi . tena amewekeka msaada tele maana yake msaada huo unasubiria wewe uitaji ili utumike maana umezidi.
Baba katika jina la yesu kristo ninaomba kila ninapo hitaji msaada kutoka kwako iwe ni fedha,mali,gari,nyumba,afya,imani,wokovu nipate kwa jina la yesu ameni.   zaburi:60: 12  Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
vi)Wakati wa mateso

ninafahamu kila mwanadamu anapita katika mateso ila bila msaada na kukimbilia kwa mungu kutuondoa katika mates ohayo hatuwezi kushinda hata kidogo. Na wala hatuwezi kuondoka katika mateso ya dunia hii isipokuwa kwa msaada wa mungu msisitizo wangu kwako ni wewe kujua kuwa mungu ni msaada kwako ukisha mwamini na kumfanya kuwa wako, anza kumfanya kuwa ni msaada kwako na kuwaambia wengine msaada wamungu upo kwa matendo makuu akutendeayo baada ya kumwamini. Ninakuona ukitembea kwenye viwango vya msaada wa mungu isivyo kwaida ninamwona bwana akifanya kwako kwa kiwango cha juu sana ukimwamini na kumkimbilia huyu bwana wa majeshi asiye shindwa na lolote. Nahumu1: 9  Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.
10  Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.


      i.            Hatutaogopa ijapo badilika nchi
Mtu aliye okoka anao ulinzi wa bwana hata yangetokea magumu yakutisha yeye haogopi kwahiyo nakutia moyo usiogope usiogope isaya41: 10  usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Mungu akutie ujasiri katika kila jambo ufanyalo usiogope majaribu maana yapo kwa kadiri ya imani yako wala huta anguka kabisa wala hayata kushinda maana bwana ni kimbilio lako na ni uzima wako katika jina la yesu roho ya hofu naiondoa kwako.

No comments:

Post a Comment